Error loading page.
Try refreshing the page. If that doesn't work, there may be a network issue, and you can use our self test page to see what's preventing the page from loading.
Learn more about possible network issues or contact support for more help.
Title details for Tekeli by Msafiri J. Mwaikusa - Wait list

Tekeli

ebook

"Yesu akajibu, akawaambia, Je! Hampotei kwa sababu hii, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu?" Marko 12:24. Kutojua maandiko wala uweza wa Mungu ni tatizo kubwa sana kwa mwili wa Kristo. Na Yeremia 9:23, 24 inasema, "Bwana asema hivi, Mwenye hekima asijisifu kwa sababu ya hekima yake, wala mwenye nguvu asijisifu kwa sababu ya nguvu zake, wala tajiri asijisifu kwa sababu ya utajiri wake; bali ajisifuye na ajisifu kwa sababu hii, ya kwamba ananifahamu mimi, na kunijua, ya kuwa mimi ni Bwana, nitendaye wema, na hukumu, na haki, katika nchi; maana mimi napendezwa na mambo hayo, asema Bwana".

Hapo Bwana Mungu amejitangaza kwamba yapasa watu wamfahamu na kumjua katika maeneo matatu, mtenda wema, hukumu na haki. Wakristo wengi wanajua na kuongelea sana kuhusu wema wa Mungu, na wengi pia wanaongelea suala la haki, hasa hasa kwamba tunahesabiwa haki kwa imani. Lakini ni wachache sana wanaomfahamu Mungu kama mtenda hukumu.

Kama hujawahi kumfahamu Mungu kama mtenda hukumu siyo rahisi kuwa umemfahamu Mungu na uweza wake sawasawa, na hii imechangiwa na kutokufahamu maandiko hasahasa kwenye kipengele cha hukumu za Mungu. Kwa sababu Yesu alisema kupotea kunatokana na kutojua maandiko wala uweza wa Mungu, basi ni vema ukatumia muda wako kusoma kitabu hiki kilichobeba uchambuzi wa maandiko kuhusu utendaji wa Mungu katika hukumu. Fundisho hili litaongeza kiwango chako cha kumcha Mungu. Barikiwa!

Formats

  • OverDrive Read
  • EPUB ebook

Languages

  • Swahili